Rais Samia amewasili Jijini Dar es salaam leo akitokea nchini Misri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 12 Novemba 2021 akitokea nchini Misri baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri, Mhe. Abdel Fattah Al-Sisi.